Askofu Gwajima akamatwa na Polisi kisa uchochezi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM, limemuhoji Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa tuhuma za kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma, zenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini.
Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 3, 2020, na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, SACP Camillius Wambura, na kusema kuwa kutokana na jumbe hizo kuonekana kuhamasisha vitendo vya kikabila,Jeshi hilo limempa onyo kali la kuacha mara moja vitendo vya kuligawa Taifa.

Post a Comment

0 Comments