Watu 10 waliolipwa mabilioni kwa kupost matangazo Instagram mwaka 2019


Ni siku ya kwanza ya mwaka mpya 2020, japo mwaka 2019 tumeshaumaliza lakini sio mbaya kuendelea kuyafahamu yaliyotisha zaidi kwa mwaka huo ambapo hii ni orodha ya Mastaa 10 walioingiza pesa nyingi kupitia Mtandao wa Instagram kwa kupost tu matangazo ya biashara ya kampuni mbalimbali.
Khloe
10. Model Kloe Kardashian wa Marekani mwenye 102 million followers alipost matangazo mawili tu mwaka huu ameingiza zaidi ya Tsh. BILIONI 2.7
Ronaldhinho
9. Mcheza mpira wa kitambo Ronaldinho (50m followers) kaingiza zaidi ya BILIONI 5.6 Tsh. ambapo analipwa zaidi ya Tsh. MILIONI 500 kwa post moja.
Kylie
8. Model wa Marekani Kylie Jenner (22) mwenye followers milioni 155 aliingiza USD ambazo ni zaidi ya Tsh. BILIONI 8.7 huku akilipwa zaidi ya BILIONI 2 Tsh. kwa post moja.
Zlatan
7. Mchezaji Zlatan Ibrahimovic (40m followers) kaingiza zaidi ya Tsh. BILIONI 9 kwa kupost matangazo 38 tu.
Neymar
6. Mchezaji Neymar (130m followers) kaingiza USD ambazo ni zaidi ya Tsh. BILIONI 16 kwa kupost matangazo 10 tu. 
Selena Gomez
5. Mwimbaji wa Marekani Selena Gomez (164m followers) kaingiza zaidi ya Tsh. BILIONI 18 kwa kupost matangazo 9 tu. 
Beckham na Mtoto wake kwenye picha
4. Mchezaji wa kitambo David Beckham (44yrs) kaingiza zaidi ya Tsh. BILIONI 24 kwa kupost matangazo 30 mwaka 2019 na kumfanya awe Staa wa Uingereza alieingiza pesa nyingi zaidi kupitia Instagram. 
3. Model Kendall Jenner (24yrs) wa Marekani akiwa na followers milioni 120 ameingiza USD ambazo ni zaidi ya Tsh. BILIONI 36 kutokana na matangazo 26 tu aliyopost ambapo anachaji sio chini ya BILIONI 1 na milioni 400 kwa post moja.
Messi na Mke wake kwenye picha
2. Mcheza soka Lionel Messi (32yrs) kaingiza USD ambazo ni zaidi ya Tsh. BILIONI 53 kutokana na kupost matangazo 36 tu kwa followers wake zaidi ya milioni 139.
Ronaldo
1. Cristiano Ronaldo (34yrs) akiwa na followers zaidi ya milioni 194 kaingiza USD 47.8 million ambazo ni zaidi ya Tsh. BILIONI 109 kutokana na post 49 tu za matangazo kwenye instagram yake, je? hapo ulipo Instagram imekuingizia pesa yoyote mwaka 2019?

Post a Comment

0 Comments