Mke Auawa Kwa Risasi Na mume Wake "Wivu Wa Kimapenzi"

Beata Kafuru mkazi wa Mtaa wa NHC, Tunduru Mkoani Ruvuma,mwenye umri wa miaka 26 amefariki kwa kinachodaiwa amepigwa risasi 3 kichwani na Mchumba wake James Paul(27) mlinzi wa TAKUKURU na kufariki papohapo ndani ya nyumba wanayoishi, chanzo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
-
“Marehemu alikuwa Muuguzi Hospitali ya Wilaya Tunduru na ameacha Mtoto mchanga wa miezi 11 aitwae Aviera, mtuhumiwa anasema wameishi pamoja kwa miaka 4 hadi wakazaa na walipanga kuoana,Beata akaenda kujiendeleza kimasomo Peramiho aliporudi akabadilika na kudai hamtaki”-RPC RUVUMA
_
“Kwahiyo chanzo ni wivu wa kimapenzi na kulipiza kisasi kwasababu James anadai marehemu alikuwa anamtamkia Waziwazi kwamba hamtaki wakati alikuwa anampenda sana na hakuwa tayari kushare na mwingine, ila Binti kasema amepata mwingine na akataka waachane”-RPC RUVUMA
_
“Kabla ya tukio mtuhumiwa alikuwa lindoni Ofisi za TAKUKURU na akatoka lindoni kwenda kutimiza adhima yake, James alipoua akataka kujiua pia, lakini kumbe risasi zilikuwa zimedondoka Housegirl akamuwahi kwa kupiga kelele Askari waliokuwa Doria wakafika”-RPC RUVUMA
_
“Katika eneo la tukio tumekuta Pistol aina ya Browing (mali ya TAKUKURU), risasi nne ambazo hazikutumika na maganda matatu ya risasi, James tunamshikilia na tutamfikisha Mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Wilaya Tunduru”- RPC RUVUMA

Post a Comment

0 Comments